Tetesi za Nandy na Billnas Kurudiana, Nandy Afunguka Mazito


Msanii wa muziki wa Bongo fleva Faustina Charles ‘Nandy’ na msanii mwenzake anayefanya muziki wa hip hop William Lyimo ‘Billnas’ walirudi kwenye headlines tena na kuzua gumzo Baada ya kuonekana pamoja.

Gumzo hilo lilizuka wiki iliyopita Baada ya Nandy kiposti picha kwenye ukurasa wake wa Instagram ilimuonyesha akiwa pamoja na Billnas na msanii mwenzao Dogo Janja.

Baada ya kuposti picha hiyo maneno mengi yalisemwa ikiwemo tetesi as kwamba huenda wawili hao wamerudiana ama vipi huku baadhi ya mashabiki kuonekana kufurahia wawili hao Kuwa pamoja.

Kwenye mahojiano yake na Global Publishers Nandy alisema hana kinyongo kabisa Billnas kwani walishamaliza tofauti zao tangu zamani hivyo kwa sasa wao ni washkaji tu na hakuna kingine kinachoendelea kati yao.

Mimi na Bill sasa hivi ni washkaji tu, hakuna chembechembe yoyote ya mapenzi kati yetu, tulishaachana muda mrefu na kila mtu ana maisha yake, sioni tatizo kuwa naye karibu”.

Wawili hao walishawahi kuwa kwenye mahusiano siku za nyuma lakini walikuja kuachana na hata video yao ya faragha kusambaaa kwenye mitandao ya kijamii.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *