TANGA: Mama Wa Kambo Amchoma Kisu Mtoto Alievunja Chupa Ya Chai

Mwanamke aliyefahamika kwa jina moja la Ashura amemtendea unyama huo Mtoto wake wa kufikia kwa madai kuwa amevunja chupa ya chai

Mtoto Zainabu Hussein(8) Mwanafunzi wa Darasa la 2 katika Shule ya Msingi Changa, amesema kabla ya kuchomwa kisu hicho kiliwekwa motoni

Ameeleza kuwa Baba yake anafanya kazi Kiwanda cha Saruji na kwakuwa anarudi usiku hakupata taarifa za tukio hilo la kusikitisha alilofanyiwa Mtoto wake

Mtoto huyo akilia kwa uchungu ameomba msaada wa kupelekwa kwa Mama yake mzazi anayeishi Mkoani Dodoma

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *